FAIDA YA KUJUA KWAMBA NI VEMA KUMUTII MUNGU KULIKO WANADAMU

tuliona kwamba Mungu alijulisha watu wake siku ya kweli ya kumtolea ibada. Siku ile ni siku ya saba ya juma, yaani sabato. Ajabu ni kwamba, wanadamu wamemupinga Mungu na kujiwekea siku zingine za juma. Kwa wamoja ni siku ya kwanza ya juma ; wengine ni siku ya sita ya juma, na kadhalika.

HOME COMING

MATANDA SDA

6/29/20255 min temps de lecture

Jana tuliona kwamba Mungu alijulisha watu wake siku ya kweli ya kumtolea ibada. Siku ile ni siku ya saba ya juma, yaani sabato. Ajabu ni kwamba, wanadamu wamemupinga Mungu na kujiwekea siku zingine za juma. Kwa wamoja ni siku ya kwanza ya juma ; wengine ni siku ya sita ya juma, na kadhalika.

Kwa ujumla, watu wengi wanaabudu Mungu siku ya kwanza, ingawa hawana ushuhuda wa Biblia unao agiza mabadiliko ya Sabato. Je, tumtii nani kati ya Mungu na mwanadamu ? Leo tutaona nukta zifuatazo :

1) Mwanzo wa kushika siku ya kwanza

Kabla hatuja ingia ndani ya fundisho letu, tunawajulisha kama leo tutawaletea habari nyingi za waandishi ili tuelewe vizuri fundisho hili.

Mwandishi anaye itwa W. Duncan Eva, katika kitabu chake “Sabato ya kweli: Ijumaa, Jumamosi au Jumapili, 38-39, aliandika yafuatayo :

« Wakristo wa kale katika siku za mitume wali tunza sabato ya kweli. Kama wakati ulivyo endelea, walianza kuwa wazembe kuhusu mambo mengine ambayo injili ili amuru. Watu waliinuka kutoka katika kanisa ambao walisema mambo ya uasi. « Wengine walikuwa kama watu washenzi kati yao katika njia nyingi na walianza kuingiza desturi na mafunzo mengine ya kishenzi.

Moja ya desturi hizi za kishenzi ilikuwa ni utunzaji wa Jumapili. Wakristo wengine waliitunza siku hii, wakasema ilikuwa ni kwa kuheshimu ufufuo wa Yesu. Washenzi waliitunza kwa heshima ya Jua.

Kama wakati ulivyo endelea, siku ya kwanza ya juma iliheshimiwa zaidi, jumapili, na sabato kidogo na kidogo zaidi, sabato ile ambayo sheria ya Mungu iliwaamuru wafuasi wa Mungu kuitunza. Mara watu wengi walianza kuiangalia juma pili kama sabato, naowakafikiri kama ilikuwa ni dhambi kutumika katika siku hiyo. Kama miaka miatatu baada ya Yesu kupaa.

Constantine mfalme wa Rumi akakiri kwamba alikuwa ameanguka na kuingia katika dini ya kikristo. Yeye tena akaweka sheria kuwa watu wote katika himaya yake ingewalazimu kuiheshimu siku ya juma pili kama siku ya kupumzika. Alidhani siku hii iliwafurahisha watu wote, wakristo na washenzi. Kwa vyo vyote katika sheria yake Constantine aliita siku ya kwanza ya juma « siku takatifu jua ». Kwa hivyo wakristo waliamriwa kuitunza siku hii ya jua. Myaka fulani baadaye kanisa la katolika katika baraza la Laodicea pia likapitisha sheria ya jumapili, kukataza watu wasipumzike katika siku ya sabato (Jumamosi) na kuwaamuru kupumzika katika siu ya jumapili. » (321 AP.JC. Concile de Laodicée).

- Lakini, tukumbuke yale Mungu aliyo agiza katika Kumbukumbu 4 :1,2 « Musiongeze … wala musipunguze … »

2) Mabadiliko ya sabato yametabiriwa

- Mtume Paulo aliandika nini ? 2Watesalonika 2:3-4,7

- Paulo anazungumzia wazee wa kanisa la Efeso: Matendo 20:29,30

- Zamani kabla ya siku za Mtume Paulo, Danieli naye alikuwa ameonya juu ya mambo haya: Danieli 7:7,8, 17, 24-25.

Kubadilisha sabato kwa Juma pili, hakuna msingi wowote wa kibiblia, kwa sababu, dimanche inajulikana katika biblia kama siku ya kwanza ya juma: Matayo 28:1

Katika Biblia yote, hakuna andiko hata moja linalo shuhudia kwamba, Yesu au mitume wake waliamuru kubadili pumziko ya sabato na kuiweka kwa siku ya kwanza.

Baba Enright, Padiri mmoja wa kanisa la kirumi aliahidi kutoa pounds 1000 kwa mtu yeyote atakaye hakikisha katika Biblia kwamba dimanche ni siku takatifu ya Mungu nay a ibada. Hebu angalia ushahidi wa wasomaji mashuhuri wa Biblia:

a) Congregationalists: « Ni wazi kwamba, ingawa tunaheshimu juma pili kiasi gani, si sabato tunayo heshimu. Sabato ilianzishwa na agizo la Mungu… Hatuwezi kutumia agizo hilo kwa ajili ya jumapili (Sunday)… Hakuna shairi hata moja katika Agano jipya lisemalo kwamba tutahukumiwa kwa kutoshika hiyo jumapili inayofikiriwa kuwa takatifu. » Dr. Dale, The Ten commandments, New York, Eaton & Mains, p. 127-129

b) Kanisa la Waluteri: “Kwa sababu haikuwezekana kupata shairi hata moja katika maandiko ambalo lingeshuhudia kuwa Bwana mwenyewe au mitume wake waliagiza uhamisho wa sabato kwa siku ya kwanza ya juma, haikuwa rahisi kujibu swali hili: Nani alihamisha sabato na nani alikuwa na ruhusa?” Georges Sverdrrup, “ A new Day,” in Sunday and its observation, 1879.

c) Presbyterian: “Hakuna neon wala mfano hata moja katika Agano jipya usemao kwamba yatupasa kuacha kutumika siku ya kwanza ya juma… hakuna amri ya Mungu inayotetea pumziko la siku ya kwanza ya juma.” Canod Eyton, The Ten commandments, London: Trubner, p. 62-65

d) Anglican: “Na ni wapi maandiko yanasema kwamba tushike siku ya kwanza ya juma? Tulipewa agizo la kushika siku ya saba, lakini hakuna mahali tunaambiwa kutakasa siku ya kwanza.” Isaac William, Plain sermons on the Catechism, Vol 1, p. 334,336

e) Methodists: “Ni kweli kwamba hakuna agizo la kubatiza watoto wadogo; vile vile hakuna agizo la kutakasa siku ya kwanza ya juma. Wengi wanafikiri kuwa Kristo alibadili sabato, lakini, kufuatana na maneno yake mwenyewe, tunaona kwamba hakuja kwa ajili ya kusudi hilo. Wale wanaoamini kwamba Yesu alibadili Sabato ni kumwazia tu.” Amos Biney, Theological compendium, New York: Methodist Book concern, 1902, p. 180, 181

f) Episcopalians:”Tulifanya mabadiliko ya siku ya saba hadi siku ya kwanza, toka jumamosi hadi jumapili, kwa mamlaka ya kanisa takatifu Katolika…” Bishop Seimour, Why we keep Sunday, p. 28

g) Baptists: “Ni vigumu kwangu kueleza kwamba Yesu, katika miaka tatu aliyomaliza na wanafunzi wake akiwazungumzia kila mara kuhusu sabato,… hakusema lolote kuhusu uhamisho wa siku. Tena hakugusia jambo hilo siku 40 baada ya kufufuka kwake. Hata Roho Mtakatifu mwenyewe, kama tunavyojua, aliyetolewa kwa kuwakumbusha mambo yote, hakusema lolote. Hata mitume wenyewe, katika kuhubiri injili ya kusimamisha makanisa hawakubishana wala kuzungumzia jambo la kuihamisha siku. Kwa kawaida, ninajua vizuri, kwamba kutunza jumapili kulianza mapema katika historia ya kikristo kama tulivyofundishwa na wa baba wa kanisa na vitabu vingine. Lakini ni huzuni kwamba inachukuwa alama ya kipagani, ikabatizwa kuwa ya kikristo kwa jina la Mungu-jua, na kukubaliwa na kutakaswa kupitia uasi wa kipapa, na kuachiwa waprotestanti kama urithi mtakatifu.” Dr. E. T. Hiscox, Rapport de son sermon à la Convention des Pasteurs dans le “New York Examiner”, du 16/11/1893

h) Kanisa Katolika: « Unaweza kusoma Biblia tangu Mwanzo hadi Ufunuo, na hutapata hata shairi moja linaloagiza kutakasa jumapili. Maandiko yanaagiza kushika kikamilifu siku ya Jumamosi, siku ambayo sisi hatuishike. » Carinal Gibbond, La foi de nos pères, p. 96.

« Kufuatana na vile Biblia haiagize kushika jumapili bali jumamosi, je si ajabu kuona kwamba wale wasio wakatolika ambao hujidai kwamba dini yao inatoka kwa Biblia na sio kwa kanisa, wanashika jumapili badala ya jumamosi ? Hivyo wanajikana wenyewe. Desturi ya kushika jumapili haitokane na andiko takatifu, bali ni kwa mamlaka ya kanisa Katolika. Desturi hiyo inabaki ukumbusho wa kanisa letu mama ambalo watoto wake wasio wakatolika walijitenga nalo, kama vile mwana mpotevu aliyetoka nyumbani lakini anaendelea kuchunga picha ya mamaye mfukoni mwake au nyuzi ya nywele zake. » John Obrien, Savant catholique, The Faith of Million (1974).

« Wakatiloka na waprotestanti kwa jumla hawashike jumamosi bali jumapili. Ikiwa maandiko matakatifu ndiyo kanuni ya imani, tunaona kuwa hii ni kinyume kabisa na amri ya Mungu, kwani, kulingana na Agano la kale, jumamosi ndiyo inapaswa kutakaswa; na ni hiyo ambayo mitume walitakasa katika Agano jipya, na hatusome mahali popote katika maandiko matakatifu kwamba amri hiyo iliondolewa. Kwa hiyo, waprotestanti, yawapasa kurudia au kwa jumamosi ya wayahudi, au kutii mamlaka ya kanisa katolika ambalo kwa mamlaka lililopewa na Mungu, lilibadilisha jumamosi kwa jumapili. Na tendo hilo si utaratibu tu wa dini, bali ni kubadilisha amri ya Mungu.” Abbé Ad. Tanquerey, P.S.S., Professeur de Théologie dogmatique, Synopsis Theologicae Dogmaticae, éd. 1922, t.l, p. 368

3) Heri kwa wale wanao baki waaminifu kwa Mungu

- Wakati wa Constantino na kanisa la Kirumi, kuna watu wenginebwalio baki waaminifu wakashika sabato ya kweli

- Nasi tuna agizwa kufuasa mfano wao: Matendo 17:30,31; Yakobo 4:17; Yohana 14:21

Yawezekana kwamba ulikuwa ukishika dimanche bila kujua kama ni agizo la wanadamu. Mpaka pale haujahukumiwa. Lakini sasa, leo umesikia kwamba dimanche siyo siku ya kweli ya kupumzika. Je, utamtii nani kati ya Mungu na wanadamu? Kumbuka kwamba, “ni vema kumtii Mungu kuliko wanadamu”.

- Hadisi ya mama aliye kuwa akitengeneza pombe yam tama akakataa kutubu, mpaka kulunguzwa na pombe hiyo.

MWITO: Ni wangapi wanao amua kumutii Mungu kuliko wanadamu wakipumzika katika siku ambayo yeye mwenyewe aliamuru? Aksante.