FAIDA YA KUJUA UBATIZO WA KWELI

Leo, kuna aina nyingi za ubatizo: kuzamisha majini,kumimina, kunyunyiza maji kipajini, kuvuka mto, kupita motoni, … Swali ni hili: Je, aina zote hizi za ubatizo zina msingi wa Biblia? Kama sivyo, nini iliyo ubatizo wa kweli, na maana yake ni gani?

HOME COMING

Matanda SDA/Bienveillant

6/30/20252 min temps de lecture

Leo, kuna aina nyingi za ubatizo: kuzamisha majini,kumimina, kunyunyiza maji kipajini, kuvuka mto, kupita motoni, … Swali ni hili: Je, aina zote hizi za ubatizo zina msingi wa Biblia? Kama sivyo, nini iliyo ubatizo wa kweli, na maana yake ni gani?

Katika fundisho la leo, tutajibu kwa maswali yafuatato:

1) Ubatizo una maanisha nini?

Waroma 6:3-4; Wakolosai 2:12; 1Korinto 12:13; Matendo 2:46,47.

Ubatizo ni kaburi ambamo muamini anazika maisha yake ya kale ili apate kutembea katika maisha mapya ya kikristo. Kubatizwa ni kuanza upya tena. Ni kukomesha yaliyopita yasiyo mpendeza Bwana, na kuanza maisha ya kumtii Mungu.

Angalia mfano wa Saulo aliyeitwa Paulo

- Matendo 22:4-5: Maisha yake ya zamani

- Matendo 22:6-10: Kukutana na Yesu

- Matendo 22:11-16: Kubatizwa; kuanza upya tena!

2) Aina gani ya ubatizo inayo kubaliwa na Biblia?

Kuna aina moja tu ya ubatizo ambayo inakubaliwa na Biblia.

- Waefeso 4:4,5 (ubatizo moja)

- Yohana 3:23 (… Ainoni palikuwa maji mengi)

- Matayo 3 :16,17 (Alitoka katika maji)

Neno kubatiza linatoka kwa lugha ya kiyunani baptizein linalo maanisha kuzamisha. Hivi, ubatizo wote ambao ni kinyume na ile si ubatizo unao ambatana na asili ya neno lile.

3) Agizo la ubatizo lilitolewa na nani? Matayo 28 :19-20

Mbele ya kutoa agizo hili, Yesu anajulisha kwanza wanafunzi wake eneo la utawala wake (V ; 18,… Mamlaka yote mbinguni na duniani).

Yesu anajulisha idadi ya majina mtu anapashwa kubatizwa ndani (Baba, mwana na Roho mtakatifu). Hii inaonyesha ushirika wa nafsi hizi tatu za Mungu na umoja wazo : Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni nafsi tatu za uungu. Kwa sababu ya ushirika na umoja huo ndiyo maana Mungu ni mmoja.

Yesu anapana Amri kwa mitume wake : kubatiza ni moja wapo wa maagizo tuliopewa na Yesu.

Yesu mwenyewe alibatizwa si kwamba alikuwa na dhambi (1Petro 2 :22), bali, alipenda kutupatia mfano (matayo 3 :13-15)

4) Nani anaye weza kubatiziwa ?

Yule anaye stahili kubatizwa anapashwa kutimiza kanuni zifuatgazo :

- Afundishwe : Mariko 16 :15

- Aamini : Mariko 16 :16

- Atubu : Matendo 2 :37-38

Kufuatana na kanuni hizi, ubatizo wa watoto haukubaliwe na Biblia.

5) Kusudi mtu abatizwe inaomba muda gani ?

- Matendo 16 :30-33

- Matendo 8 :36-39 (v ; 26-39)

- Matendo 22 :11-16

Baada ya kusikia neno la Mungu na kuamini Yesu Kristo, mtu anapaswa kubatizwa.

6) Mtu aweza kubatizwa mara ya pili?: Matendo 19 :1-5 ; Yohane 13 :5 ; Yohane 16 :7-11, 13-14.

Ubatizo ni tangazo linalo shuhudia ya kwamba mtu fulani amejiunga na kundi fulani la waamini kwa sababu fulani. Hivyo, ubatizo waweza kuwa wa kweli au wa uwongo kufuatana na imani uliyo ikubali na iliyo kusukuma kuingia majini.

7) Kuna hatari gani mtu anapokataa kubatizwa?: Yohane 3 :3,5 ; Marko 16 :16b

Ndugu au dada uliye tusikiliza tangu mwanzo wa mafundisho yetu, tuna amini ya kwamba umesikia mengi, na umeamini ya kwamba ni kweli. Leo ndiyo siku ya kukubali kuonyesha imani yako ukiamua kubatizwa.

MWITO : Wote wanao kubali kujiunga na kundi la Mungu kupitia ubatizo wa kweli, wasimame tuwaombee.