FAIDA YA KUJUA HUKUMU INAYO HUSU WATU WOTE
Unahitaji Yesu akutetee hukumuni ili uhesabiwe haki mbele ya Mungu ?
MATANDA SDA
6/26/20252 min temps de lecture


tuliona kwamba, moja wapo ya sababu za kurudi kwa Yesu, ni kuja kulipa kila mtu kufuatana na matendo yake. Hii ina maanisha kama maisha yetu kwa jumla yanachunguzwa. Ni lazima uchunguzi huu ndio uonyeshe kama, mtu fulani anastahili uzima wa milele au mauti ya milele.
Leo tutajifunza nukta zifuatazo :
1. Uhakika wa hukumu ya Mungu kwa wanadamu: 2Wakorinto 5:10; 1Petro 4:17
Kwa kawaida, hukumu ina pande mbili: kuhesabiwa haki, na kupewa azabu. Tunapofikiria hukumu, tusiutazamie ule upande moja tu wa kupewa azabu (condamnation), au pengine ule wa kuhesabiwa haki tu, bali, pande zote mbili. Maisha na uamzi wa kila mmoja wetu, ndivyo vitakavyo muweka kwenye upande fulani.
2. Vyombo vya ushuhuda katika hukumu
a. Shahidi wa kwanza: MUNGU. Medhali 15:3 “Macho ya Bwana ni katika kila pahali, yakitazama wabaya na walio wema”. Matendo 17:30,31
b. Shahidi wa pili: VITABU. Kuna vitabu vya aina tatu:
- Kitabu cha ukumbusho : Malaki 3 :16
- Kitabu cha uzima : Ufunuo 20 :12
- Kitabu cha maovu : Yeremia 2 :22 ; Zaburi 56 :8
c. Shahidi wa tatu : WAMALAIKA. Kila mtu ana malaika mlinzi anayetoa taarifa ya matendo yake : Matayo 18 :10
d. Shahidi wa Ine : DHAMIRI YA MTU
3. Mambo yanayo chunguzwa hukumuni
a. Matendo: Ufunuo 20:11,12b; Ufunuo 22:12
b. Maneno: Matayo 12:36,37
c. Mafikiri au mawazo: 1Wakorinto 4:5
d. Makusudi (les mobiles, les intentions): Medhali 16:2
Mfano wa mume (muongozi) aliye kuwa akisaidia mama mukimbizi tena mjane akiwa na nia ya kumuoa ili awe mke wa pili.
4. Kanuni ya uchunguzi na hukumu au “Code de justice de Dieu”
Katika kila kesi, kunakuwa kanuni za hukumu au code de loi. Ni kitabu cha sheria. Kama sheria fulani imevunjwa, kumetayarishwa azabu fulani. Kama mutu ameshika sheria hizo, anahesabiwa haki, na kuachiliwa huru. Katika hukumu ya Mungu, kanuni ni AMRI kumi zake. Mhubiri 12:13,14 (au 15,16); Yakobo 2:12,13
5. Matayarisho kuhusu hukumu : 1Yohane 2 :1,2 (Mtetezi wetu ni Yesu)
- Kwa watu walio samba, wakati mutu ana kesi, anafanya awezavyo ili aelewane na Avocat wake
- Tunayo bahati kubwa sana, sababu avocet wetu hatulazimishe RUSHWA. Anatuomba tu tukubali kumubebesha mizigo yetu (Matayo 11:28), tumuache awe mtawala wa maisha yetu. Mambo mengine, atayakamilisha.
MWITO: Unakubali Yesu atawale maisha yako tangu leo? Unahitaji Yesu akutetee hukumuni ili uhesabiwe haki mbele ya Mungu ? Ikiwa ndilo hitaji lako,
Mungu akubariki.