FAIDA YA KUJUA UHUSIANO ULIOPO KATI YA SHERIA NA NEEMA
Watu wengi wametoa maoni mbalimbali kuhusu neema na sheria. Wamoja wanasema kwamba, sababu tumeokolewa kwa neema, hatupaswi kushika sheria. Wengine wanasema, usiposhika sheria, hauwezi kuokolewa.
HOME COMING
MATANDA SDA
6/27/20252 min temps de lecture


Watu wengi wametoa maoni mbalimbali kuhusu neema na sheria. Wamoja wanasema kwamba, sababu tumeokolewa kwa neema, hatupaswi kushika sheria. Wengine wanasema, usiposhika sheria, hauwezi kuokolewa.
Maoni haya yamesababisha wengi kufikiri kama NEEMA ya Mungu inapingana na SHERIA zake. Ndiyo maana, tulipenda kutoa fundisho hili, ili kwa msaada wa BIBLIA, tuweze kuelewa uhusiano kati ya NEEMA na SHERIA, ambayo ni kama “Wadada wawili wasio weza kuachana.”
Katika fundisho hili tutaona mambo yafuatayo:
1. Nafasi ya NEEMA, kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu
Neema ni nini? “Yule anaye ishi chini ya Neema ni yule aliye kubali msamaha wa dhambi zake kwa imani katika kafara ya Kristo, na aliye pokea msamaha huo kwa bure bila kufanya matendo mazuri”
Mwanadamu amestahili msamaha wa dhambi tangu wakati gani? Mwanzo 2:15-17; 3:4-19 (Alitenda dhambi kwa kuasi: 1Yohane 3 :4 « … Dhambi ni uasi ».
Mungu alitoa msamaha huo kwa njia gani ? Kwa bure = NEEMA (Mwanzo 3 :15, 21).
Soma waroma 3 :23-26
Neema hii iliendelea kuonekana, tangu Adamu, kwa wakati wa Nuhu (Mwanzo 6 :5-8), na uzao wake.
- Kuchaguliwa kwa Abramu, kulikuwa kwa neema pia ; uzao wake, mpaka wakati
Yesu alipo zaliwa.
Hivyo Neema ya Mungu haikuanza tangu Yesu anapokuja duniani, bali, tangu mwanadamu ameanguka dhambini.
2. Nafasi ya SHERIA kuhusu uhusiano wa Mungu na mwanadamu
- Sheria za Mungu ni musemo wa tabia zake « La loi de Dieu est l’expression de son caractère »
- Kupitia sheria, Mungu ameonyesha yale anayo yapenda, na yale anayo kataa
- Sheria za Mungu, zinapatikana katika maisha ya viumbe vyake vyote: “ Lois naturelles”
Mfano:
Katika sayari (ona dunia inayo zunguka kwenye yeye peke (24h), na kwenye jua (365 jours & 6h)
Kukomaa kwa mimea
Kupumua kwa mwanadamu na kadhalika
Jua kutoa mwangaza mchana, mwezi kutoa mwangaza usiku. Ona tetemeko la ardhi na matukio yake
- Adamu na Eva waliasi sheria, wakatendadhambi
- Sheria au Amri za Mungu zinajulikana kwa idadi gani?
Amri kumi: décalogue = Déca (10), logos (maneno)
Maneno kumi, au Amri kumi
- Amri hizi zinapatikana katika Kutoka 20:3-17
- Amri hizi zimetolewa kwenye mbao mbili za mawe; kwenye ubao moja kukiwa Amri ine (4), kuhusu mwanadamu na Mungu; kwenye ubao wa pili, Amri sita (6) kuhusu mwanadamu na mwenzake. Kutoka 31:18; 32:15,16
Amri hizi kumi, Yesu amezieleza kwa kifupi katika Matayo 22:34-40. Yesu alishika amri zote: Matayo 5:17-19.
3. Uhusiano wa NEEMA na SHERIA katika mpango wa Mungu wa kuokoa mwanadamu
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya Neema na Sheria
Yakobo 2:14-26
Wagalatia 3:24-26
2Wakorinto 5:17
Waroma 6:1,2,12-14
Waroma 7:7-13; 6:19-21
Tito 2:11-15
Neema na sheria ni dada wawili wasioachana. Tumekombolewa kwa neema,kwa njia ya Imani katika kafara ya Yesu Kristo. Neema hii, inapojulikana, inakubaliwa. Huo ukubali ndiyo Imani. Yule anaye kuwa na imani ya kwamba amekombolewa kwa neema, ataishi maisha ya shukrani kwa Yule aliye mkomboa yaani Yesu. Mapenzi ya Yesu ni kushika Amri zake (Yohana 14:15).
MWITO: Je, una imani ya kwamba umekombolewa kwa neema? Unapenda kuhakikisha imani hiyo ukiionyesha kwa njia ya matendo ya shukrani kwa mkombozi wako Yesu Kristo? Je, ungependa Yesu akuwezeshe kumpenda unapo shika amri zake? Ikiwa ndilo hitaji lako, Mungu akubariki sana.