FAIDA YA KUJUA HESHIMA INAYO MSTAHILI MUNGU
Duniani kuna watawala wengi; watawala hawa wana vyeo tofauti. Kila mtawala anapewa heshima kufuatana nadaraja la cheo chake. Cheo cha kutolea mmoja kinaweza kuwa tofauti ya cha mwengine kufuatana na utofauti wa vyeo vyao.
HOME COMING
MATANDA SDA
6/28/20251 min temps de lecture


Duniani kuna watawala wengi; watawala hawa wana vyeo tofauti. Kila mtawala anapewa heshima kufuatana nadaraja la cheo chake. Cheo cha kutolea mmoja kinaweza kuwa tofauti ya cha mwengine kufuatana na utofauti wa vyeo vyao.
Sasa Mungu anaye tawala mbingu na dunia na viumbe vyote vilivyomo, anastahili heshima gani?
Katika fundisho la leo tutaona nukta zifuatazo:
1. Mungu anatudai heshima gani?
- Mungu anatudai IBADA TAKATIFU: Ufunuo 14:6,7
- Namna ya kutoa ibada hiyo : Kutoka 20 :8-11
- Mungu ameonyesha umuhimu wa ibada hii tangu mwanzo : Mwanzo 2 :1-3
- Agizo hili lilitolewa kwa watu wote : Kutoka 31 :15 ; Kutoka 16 :4,5, 22-26, 27, 28-30 ; Isaya 56 :1-7 ; Marko 2 :27
- Alama ya utakaso, na Agano ya Mungu na watu wake : Ezekiel 20:12,20; Kutoka 31:17
- Agizo hili liliheshimiwa na Yesu mwenyewe : Marko 2 :28 ; Luka 4 :16 ; Luka 23 :24 ; 23 :55,56
- Mitume walishika agizo hilo : Matendo 13 :14 ; 17 :1,2 : 18 :4 ;13 :42,44
Watu wana namna tofauti ya kutoa heshima:
- Kuvua kofia kichwani
- Kutoa mikono miwili
- Kuinama (ona wake wa Uganda): Je, ikiwa wanadamu wana hitaji aina Fulani ya kuonyesha heshima, sasa kwa Mungu ni vipi? Vivyo ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu. Kumuabudu siku ingine isipokuwa ile aliyo amuru, hatakubali kama hiyo ni heshima inayo mustahili.
2. Hatari kwa wale wanao kataa kumtolea Mungu heshima inayo mustahili: Yakobo 2:10,11
Wale wanaosema kama sheria zimekwisha, mara nyingi wanagombanisha sana sabato. Si vyepesi kwao kufundisha watu kuiba, kuua, kuzini, kuzarau wazazi; lakini wana subutu kuhakikisha kwamba sabato imekwisha! Wasome vizuri Yakobo 2:10,11; 1Yohane 2:4-6; 1Yohane 5:2,3; Matayo 5:17-19.
3. Mibaraka kwa wanao mtolea Mungu heshima inayo mustahili
- Wana salama: Zaburi 119:165; Isaya 48:18
- Mungu anawafurahisha na kukubali ibada yao: Isaya 56:6,7 (ona pia Waroma 3:29-31).
Muumbaji wetu anatuomba kumtolea ibada takatifu. Kwa sababu ni yeye aliye wekanyakati, ametujulisha waziwazi siku ya kumtolea ibada hiyo. Ni siku ya saba ya juma, sabato ya Bwana.
MWITO: Wangapi wanakubali kumuheshimu Mungu wakishika sabato aliyo agiza ? Aksante.