FAIDA YA KUJUA TUMAINI LA WATU WA MUNGU
Yesu atakuja lini ? kurudi kwa Yesu Kristo ni tumaini kubwa sana. Tumaini hili, lime sababisha wengi kuacha mambo fulani ya dunia hii ambayo yangeweza kuwapa faida
MATANDA SDA/Bienveillant
6/25/20252 min temps de lecture


Tumaini ni nguvu inayo leta mvuto kwa kazi fulani au katika maisha fulani. Watu wengi wameweza kutimiza mipango ya ajabu sababu wana tumaini:
- Wanafunzi shuleni
- Wakulima shambani
- Wachuruzi safarini
- Na wengine.
Kwa watu wa Mungu, kurudi kwa Yesu Kristo ni tumaini kubwa sana. Tumaini hili, lime sababisha wengi kuacha mambo fulani ya dunia hii ambayo yangeweza kuwapa faida. Wanafanya hivi ili waweze kungojea mwokozi wao Yesu Kristo.
Katika fundisho la leo tutajibu kwa maswali yafuatayo :
1. Yesu atarudi siku gani?
Uhakika wa kurudi kwake: Yohane 14:1-3. Yesu atarudi siku gani? Matayo 24:3,36; Matendo 1:6,7. Kuna watu ambao walijaribu kuweka tarehe ya kuja kwa Yesu. Ni kama hawa:
a. JURIEU: Aliwaza Yesu atakuja mwaka wa 1785
b. BENGEL: Aliwaza Yesu atakuja kati ya myaka 1836
c. MILLER: Aliwaza Yesu atakuja mwaka wa 1843-1844
d. RUSSEL: Aliwaza Yesu atakuja mwaka wa 1874
e. GRATTAN GUINNES: Aliwaza Yesu atakuja mwaka wa 1920
f. DAVIDSON: Aliwaza Yesu atakuja mwaka wa 1936
Hawa wote, walitambua kwamba walijidanganya. Yesu alikuwa amesema:”Hakuna mtu anayejuwa habari za siku ile…” Matayo 24:26.
Hata kwa myaka iliyopita hapa nyuma, watu wengine walisema kama Yesu atarudi kwenye mwaka wa 2000. Lakini Yesu hakurudi mwaka huo.
Ila, ingawa hatujue siku wala saa ya kuja kwa Yesu, tunapaswa kukumbuka maandiko yafuatayo: Habakuki 2:3; Matayo 25:13.
2. Yesu atarudi namna gani?
a. Yesu atarudi kibinafsi: Matendo 1:11
b. Yesu atarudi wazi wazi, kwa ulimwengu wote: Ufunuo 1:7; Matayo 24:27
c. Yesu atarudi na utukufu: Matayo 25:31
3. Yesu atarudi sababu gani?
a. Kulipa kila mtu kulingana na matendo yake: Ufunuo 22:12
b. Kukusanya wateule wake: Matayo 24:31. Waaminifu walio kufa na walio hai, wote watamulaki (1Watesalonike 4:16,17
- Itakuwa furaha kwa waaminifu: Isaya 25:8,9
- Itakuwa kilio kwa waovu: Ufunuo 6:15-17
4. Yesu anatuomba kufanya nini tunapongojea kurudi kwake? 2Petro 3:14; Waroma 13:12,13; 1Yoane 2:28.
Mfano: Msichana aliye chumbiwa, baadaye aliacha kujisafisha. Wakati bwana arusi wake alipofika alimuacha, akabeba mdogo wake aliye kuwa tayari.
MWITO: Je, unaamini kwamba Yesu atarudi kuchukua wateule wake? Kurudi huko ni tumaini la Baraka kwako? Unahitaji Yesu ajapo akukute katika kundi la wateule wake ? Fanya angalisho ili usuje ukaudharau upendo wa Mungu unao kuomba kujiandaa kikamilifu. Kama ndilo hitaji lako, Mungu akubariki.